SHINDANO LA CORONA: (CORONA CHALLENGE)

Je? Wewe ni mbunifu, mwana sayansi au mjasiriamali na una miaka kati ya 7 na 12?

 

Shiriki kwenye shindano letu la ubunifu, kwa ajili ya kupata usuluhishi wa matatizo yanayotokana na janga la virusi vya Corona. Washindi watapata vifaa vya ubunifu kutoka Jenga Hub, pamoja na nafasi ya kutambulika kwenye tovuti yetu na kurasa zetu kwenye mitandao ya kijamii.

Jenga Hub, ni taasisi iliyoanzishwa kwa ajili ya kuwawezesha watoto na vijana kupata mafunzo ya kiteknolojia na kidijitali, yanayowaandaa kwa ajili ya ulimwengu wa teknolojia unaoendelea kubadilika hasa kupitia mafunzo na kazi zijazo. Jenga hub kwa kushirikiana na Designathon Works, wanafuraha kukuletea shindano hili la CORONA CHALLENGE, kuwapa fursa watoto na vijana kushiriki katika mijadala pamoja na kupata ufumbuzi wa matatizo yanayotokana na janga la virusi vya Corona.

MAWAZO MACHACHE YA KUKUPA MSUKUMO:

KWANINI USHIRIKI?

 • Una muda wa saa moja na unaweza kutumia muda huo. Una wasiwasi kuhusu matatizo ya virusi vya Corona.

 • Una mawazo mazuri na unaona ni muhimu wazo lako lisikike.

 •  Washindi watapata vifaa vya ubunifu kutoka Jenga Hub, pamoja na nafasi ya kutambulika kwenye tovuti yetu na kurasa zetu kwenye mitandao ya kijamii.

INAFANYAJE KAZI?

Jisajili pamoja na mzazi au mlezi wako. Baada ya kujisajili, utaweza kuendelea kufanya kazi yako mwenyewe.

 

HATUA YA KWANZA: Tazama Video.

HATUA YA PILI: Buni na kuchora wazo lako kwa kutumia karatasi ya kuchora.

HATUA YA TATU: Tuma mchoro wako, kwa kupakia, (Upload) ili kuingia kwenye mashindano.

KWANINI SHINDANO HILI NI LA KIPEKEE?

 • Utalazimika kutumia ubunifu wako kupata majawabu ya changamoto za dunia, ikiwemo la mlipuko wa virusi vya corona.

 • Utajiunga na kuwa sehemu ya mtandao wa ‘Watoto kwa ajili ya ulimwengu bora’.

 • Suluhisho lako linaweza kutumika nyumbani kwenu, mtaani kwako au kwenye jamii yako.

 • Mshindi atapata vifaa vya ubunifu kutoka Jenga Hub, pamoja na nafasi ya kutambulika kwenye tovuti yetu na kurasa zetu kwenye mitandao ya kijamii.

Mradi huu umewezeshwa kwa msaada wa:

Jenga Hub.png
DW-logo_new-RGB.png

Kwa kushiriki kwenye designathon mtandaoni, unakubaliana na vigezo na masharti yetu

Je? Unataka kufahamu zaidi kuhusu mfumo wa Designathon? Bonyeza hapa.

Designathon Works Foundation

Keizersgracht 264
1016 EV Amsterdam

The Netherlands

CoK: 60140615
RSIN: 853781606
Bank: NL77 TRIO 0197 9551 85

SDG-House_Amsterdam_2019_L_rgb.png
hundred_stickers_sustainability_purple.p
selected_hundred_purple.png
SNF primary logo_long_hi.jpg
Catalyst logo without tagline 80px high
One Family Foundation_big.png
 • Facebook - White Circle
 • Twitter - White Circle
 • Instagram - White Circle
 • Flickr - White Circle
 • YouTube - White Circle
 • LinkedIn - White Circle

© 2020 by Designathon Works. All rights reserved.